JINSI YA KUPIKA UBUYU ♦️MAHITAJI 👉 Sukari vikombe 2 👉 Maji vikombe 2 👉 Nusu kikombe unga wa ubuyu 👉 Vikombe 4 ubuyu wenyewe 👉 ¼ Kijiko cha pili pili ya unga 👉 ¼ Kijiko cha chumvi 👉 ¼ Kijiko cha iliki ya unga 👉 Rangi nyekundu au yeyote utakavyopenda. ♦️JINSI YA KUTENGENEZA 1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri. 2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu. 3. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena....
Hello. Karibu katika blog yetu. Je unapenda kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na afya pamoja na habari nyingine tofauti. Basi utafahamu kupitia blog yetu. Ahsanteni. Hello. Welcome to our blog. Do you like to learn various things related to health as well as other different information. Then you will know through our blog. Thank you
Comments
Post a Comment