Skip to main content

JINSI YA KUPIKA UBUYU

JINSI YA KUPIKA UBUYU

♦️MAHITAJI
👉 Sukari vikombe 2
👉 Maji vikombe 2
👉 Nusu kikombe unga wa  ubuyu 
👉 Vikombe 4 ubuyu wenyewe 
👉 ¼ Kijiko cha pili pili ya unga 
👉 ¼ Kijiko cha chumvi
👉 ¼ Kijiko cha iliki ya unga
👉 Rangi nyekundu au yeyote  utakavyopenda.

♦️JINSI YA KUTENGENEZA

1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki.  Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri. 

2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.
Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu. 

3. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.  

4. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu. 

5. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.


Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kupika Half cake

 Jinsi ya kupika Half cake Mahitaji Unga wa ngano kikombe 1na1/2 (kama robo hivi) Sukari 1/4 kikombe Baking powder 1/2 kijiko cha chai Magadi soda (bicarbonate soda/baking soda) 1 kijiko cha chai Mafuta 2 vijiko vya chai Mafuta ya kukaangia Maji ya uvuguvugu kiasi Matayarisho Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande (hakikisha unakuwa mgumu) Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi) Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke. Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani. Zikisha iva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili zichuje mafuta. Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa. dondoo muhimu:-👇👇👇👇👇 Jinsi ya kupika half keki zilizo pasuka na kuiva vizuri. 1.Hakikisha unatumia vipimo sahihi bila kusahau bicarbonate of soda(baking soda) hiki ndicho kiungo muhimu ktk half cake na baking powder...(hamira SI lazima kuweka kwa half cake za...